المدة الزمنية 3:3

DC MAGANGA ACHARUKA JUU YA SAKATA LA MAZINGIRA

بواسطة KAHAMA TV ONLINE
44 مشاهدة
0
0
تم نشره في 2021/12/07

MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA MWALIMU JOSEPHAT MAGANGA AAGIZA MSAKO WAHARIBIFU WA MAZINGIRA. Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Mwalimu Josephat Maganga ameuagiza uongozi wa kijiji na kata ya Berege kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji na kata hiyo kufanya msako kabambe kuwasaka watu wanaojihusisha na uharibifu wa Mazingira ikiwemo ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa pamoja na kuchoma misitu ovyo hali ambayo itapelekea kuwa jangwa katika eneo hilo. Agizo hilo amelitoa katika mkutano wa hadhara kata ya Berege Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wenye lengo la kujadili hali ya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji ovyo wa miti ya asili uliokithiri katika kata hiyo. Mkuu huyo wa wilaya amesema ofisi yake tayari ina orodha ya watu wanaoharibu mazingira katika Wilaya ya Mpwapwa hivyo amewataka viongozi kata ya Berege kuonesha ushirikiano ili waweze kushughulikiwa . Awali wakielezea kero zinazowakabili katika kata hiyo,Hussein Kamwaya pamoja na Diwani wa kata ya Berege Baraka Habari wamesema kero kubwa iliyopo ni ukataji wa miti hali ambayo imesababisha uoto wa asili kuanza kutoweka kwenye milima ya Berege ambapo pia kuna changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye eneo hilo. MWISHO. USISAHAU KU SUBSCRIBE CHANNEL YETU ILI UWE UNAPATA UPDATE MPYA KILA TUNAPO WEKA HABARI MPYA WAKATI WOWOTE BONYEZA HAPA CHINI KWENYE MAANDISHI YA BLUU /channel/UCcCo ... https://www.instagram.com/kahamatvonline/ #KAHAMATVONLINE #HABARIZAHIVIPUNDE

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0